24 Oktoba 2014 - 17:04
Putin: Marekani inavunja amani ya dunia

Baada kimya kirefu rais wa Urusi asema kuwa: Marekani inavunja amani ya dunia kwa kuwasaidia na kuwahami magaidi wa Daesh.

Baada kimya kirefu rais wa Urusi asema kuwa: Marekani inavunja amani ya dunia kwa kuwasaidia na kuwahami magaidi wa Daesh.
Vradmir Putin aliongeza kusema kuwa:Kuna hitajika umoja wa ukweli wenye nia ya kupambana na magaidi, na umoja ambao unahami makundi ya kigaidi.
Ni muhimu kuashiria kwamba Marekani na washirika wake ambao ndio walokuwa wakiwa shajiisha na kuwasaidia magaidi wa Daesh kupambana dhidi ya serikali halali ya Bashar asad ya Syria tangu mwaka 2011, na sasa wamegeuka na kuunda muungano wa kupambana dhidi ya magaidi hao, pia imeripotiwa kuwa ndege za Marekani zimeshusha shehena za silaha kwa magaidi wa Daesh, Jeshi la Marekani limejitetea kwa kusema kuwa shehena hizo zilikuwa ni msaada wa silaha kwa wapambani wa Kikurd lakin kwa bahati mbaya baadhi ya silaha hizo zimeshushwa katika maeneo ya magaidi hao.
Urusi na Iran ni nchi ambazo zilitangaza wazi kuuhami utawala halali wa serikali ya Syria.